Henrik Mkhitaryan (kushoto) na Mesut Ozil wote wakishangilia baada ya kuifungia Arsenal katika ushindi wa 5-1 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Emirates. Ozil alifunga dakika ya nne na Mkhitaryan akafunga dakika ya 27, kabla ya kutoa pasi za mabao mengine yaliyofungwa na Laurent Koscielny dakika ya 47 na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 59, huku bao la tano likifungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 78, wakati bao pekee la AFC Bournemouth lilifungwa na Lys Mousset dakika ya 30. Arsenal sasa inafikisha pointi 56 katika nafasi ya tano nyuma ya Tottenham Hotspur yenye pointi 60 baada ya wote kucheza mechi 28