Baada ya kupokea kipigo cha ambao 3-0 dhidi ya Azam FC juzi kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, Katibu wa Tawi la Yanga, Kjitonyama, Shamte Ally, amesema mashindano hayo hayana mvuto.
Kwa mujibu wa Radio One, Ally ameeleza kuwa kwa mwaka huu kidogo kumekuwa hakuna ushindani wa maana kutokana na aina ya timu zilizopo hivi sasa.
Ameeleza hakuna timu ambazo zimetokea nje ya nchi zaidi ya Simba, Yanga na Azam FC ambazo walau zimeleta morali kwa mashabiki visiwani humo.
Katibu huyo amesema kutokuwepo kwa timu za nje kama KCCA kumedhorotesha ushindani wa maana kama ilivyokuwa mwaka jana na iliyopita.
Kiongozi Ally anaamini pia kitendo cha timu kama Yanga kupeleka kikosi cha pili ni uhalisia wa michuano kukosa hadhi kubwa kama yaliyopita.