THOMAS ULIMWENGU AFUNGUKA MENGI KUHUSU SIMBA




Mtanzania Thomas Ulimwengu, ametua nchini na kikosi cha JS Saoura cha Algeria tayari kuwavaa Simba.

Kikosi hicho kutoka Algeria, kina kibarua dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi na mechi itapigwa kesho.

Ulimwengu mwenye uzoefu na michuano hiyo ameonyesha kuwa mtulivu na mwenye tabasamu bashasha.

Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Ulimwengu alisema: "Nina furaha kurudi kucheza tena nyumbani, Simba ni timu nzuri lakini sisi tumejiandaa kwa ajili ya kupambana nao."

JS Saoura watacheza na Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

LihatTutupKomentar