WCHEZAJI HAWA WAGOMEA MAZOEZI

Wachezaji timu TPL wagoma atokea mmoja tu mazoezini na kesho mechi

Ukisikia hali ni ngumu hakika hali ni ngumu kwa vilabu vya ligi kuu soka ya Tanzania bara hasa timu nyingi kukosa pesa ya ya mdhamini mkuu kama ilivyokuwa awali.

Moja kati ya timu ambayo hali inaonekana kuwa ngumu zaidi ni timu ya Biashara United ya mkoani Mara ambayo inaelezwa wachezaji wake wote wamekuwa hawatokei mazoezini kwa siku takribani tatu mpaka jana

Wakigoma kushinikiza kulipwa mishahara ya miezi minne huku katika mazoezi ya jana kipa Nurdin Barola pekee akitokea mazoezini.

Hali hiyo msomaji wa mkomesportnews  inatokea wakati ambao kesho Timu ya Biashara United inatakiwa kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ya mkoani Mwanza.

LihatTutupKomentar