RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA LEO


Ligi Kuu soka ya Tanzania bara TPL itaendelea kwa mechi 4 kuchezwa siku ya Jumapili 2 December 2018 katika nyasi za viwanja mbalimbali.

Katika uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo kutakuwa na Mchezo kati ya JKT Tanzania watakaokuwa wenyeji wa Ruvu Shooting mechi ikianza saa kumi kamili alasiri.

Nao Lipuli Fc ya Mkoani Iringa itakuwa nyumbani katika uwanja wa Samora kuwakaribisha Biashara United kutoka mkoani Mara kuanzia majira ya saa kumi kamili alasiri.

Kagera Sugar wanaofundishwa na Kocha Maxime watakuwa wenyeji wa Alliance Fc iliyochini ya Kocha Malale Hamsini nayo ikianza saa kumi alasiri.

Ndanda wana kuchele msomaji wa Kwataunit.co.ke watakuwa wenyeji wa Mbao Fc waliosafiri zaidi ya Kilomita 1600 kutoka Mwanza mpaka Mtwara katika mchezo utakaochezwa majira ya saa kumi alasiri Nangwanda Sijaona.

LihatTutupKomentar