Mchezaji mkongwe wa Simba Abdallah Kibadeni, ameibuka na kulitaka benchi la ufundi la Simba kufanya marekebisho kwenye safu ya ulinzi.
Kibadeni ameeleza hayo baada ya kuona mapungufu hayo kwa mechi za hivi karibuni haswa kwenye michezo ya kimataifa ikiwemo wa mwisho dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia.
Katika mechi hiyo Kibadeni ameeleza bado safu ya ulinzi haijakomaa vizuri jambo ambalo linapelekea kupata shida pale wanaposhambuliwa na wapinzani.
Kwa mujibu wa radio One, Kibadeni amesema ni wakati mwafaka wa benchi hilo kufanya maujanja ili kukifanya kikosi kiwe kamili kutokana na madhaifu ambayo yanaoneshwa na beki hiyo.
"Katika safu ya ulinzi ya Simba bado kuna madhaifu mengi, ni muda mwafaka wa benchi la ufundi kuangalia namna ya kurekebisha tatizo hilo ili kutoleta hatari ya kuruhusu mabao haswa katika mashindano ya kimataifa" alisema Kibadeni