YANGA YAPATA NGUVU MPYA



Kikosi cha Yanga kimezidi kupanuka zaidi baada ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi kuanza kurejea kwa ajili ya mazoezi.

Beki Andrew Vincent maarufu kama Dante jana alirejea mazoezini sambamba na Ibrahim Ajibu ambaye naye alikuwa mgonjwa.

Dante amerudi baada ya kumaliza adhabu yake kutokana na kitendo cha kumpiga kichwa mchezaji wa Simba, Mohammed Hussein katika mechi iliyozikutanisha timu hizo katika mchezo wa mwisho wa ligi.

Aidha, uongozi umesema kuwa mchezaji Juma Mahadhi bado anaendelea na matibabu huku akianza mazoezi mepesi.

Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi utakaopigwa wikiendi hii dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

LihatTutupKomentar