YANGA YAFUNGUKA KUHUSU HAYA SIMBA

Uongozi wa timu ya Yanga umewatupia dongo kimtindo timu ya Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga, wakiwa na mabao 23  tofauti ya mabao 6 na Yanga wenye mabao 17  ambapo wote wana pointi 26.

Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mipango kwa timu inaendelea vizuri na amewatupia dongo kimtindo wapinzani wao Simba ambao wamezidi mchezo mmoja na kuwa sawa kwenye pointi.

"Tunastahili kuitwa mabingwa wa kihistoria kwa kuwa rekodi zetu hazijafikiwa na timu yeyote, msijisahau sana, pointi sawa mmezidi mchezo mmoja," alisema.

Simba wamecheza michezo 11 kwenye ligi huku Yanga wakiwa wamecheza michezo 10 na wana mchezo mmoja mkononi.

LihatTutupKomentar