NGONO YAMUWEKA MCHEZAJI HUYU PABAYA KMC


Klabu ya soka ya KMC imeachana na nyota wake Abdulhalim Humud, kwa kile kilichoelezwa utovu wa nidhamu pamoja na kuwafanyia vitendo visivyo na maadili wachezaji wenzake.

Hilo limebainishwa leo na Katibu Mkuu msaidizi wa KMC Walter Harrison wakati akiongea na wanahabari ambapo ameweka wazi kuwa Humud amekuwa mtovu wa nidhamu na kufanya vitendo ambavyo si vya kiungwana hivyo wamefikia muafaka wa kuachana naye.

''Alianza kukosa nidhamu mbele ya mwalimu muda mrefu ikiwemo mechi ya Septemba 1, 2018 dhidi ya Coastal Union huko Tanga ambapo alikuwa mchezaji wa akiba lakini alipoambiwa ajiandae akamjibu kocha kuwa amesahau vifaa jijini Dar es salaam'', amesema.

Aidha Harrison amefafanua kuwa baada ya tukio hilo Humud alisamehewa lakini baada ya muda akafanya tukio jingine kwa wachezaji wake ambalo sio la kiungwana kwa kuwasumbua wake na wapenzi wa wachezaji wenzake ndani ya KMC na nje.hivyo kuonesha jinsi gani sio muungwana.

''Kwasababu za kimaadili sitaelezea kwa undani vitendo hivyo lakini hakufanya kwa mchezaji mmoja bali kwa wengi na alipewa onyo akakubali kubadilika lakini cha ajabu kabla hata hajaendelea akaomba kuachwa na sisi tumeridhia kuachana naye'', ameongeza.

Licha ya kuachana naye lakini KMC wamesisitiza kuwa wanasheria wa klabu hiyo watafuatilia jinsi gani watapata fidia za gharama walioingia kwake ikiwemo pesa za usajili na mishahara kwasababu tangu asajiliwe Julai 1, 2018 alikuwa bado hajaitumikia ipasavyo timu hiyo.

LihatTutupKomentar