KANGI LUGOLA AFUNGUKA HAYA KUHUSU KIPIGO CHA TAIFA STARS4


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameibuka na kuzungumzia kipigo walichokipata Taifa Stars dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu kuelekea AFCON mwakani.

Lugola ambaye ni mdau wa michezo, amesema matokeo ya kufungwa bao 1-0 na Lesotho yamewasikitisha wengi, jambo ambalo limesababisha kila mtu kuja na kauli yake.

Waziri amefunguka kuwa ni aibu kwa Stars kupoteza licha ya kupewa shilingi za kitanzania milioni na Rais John Pombe Magufuli kama motisha lakini mwisho wake timu ikafungwa.

Lugola ameamua kuja na mbinu mbadala ya kuwataka wadau na mashabiki wa Stars kupiga dua na sala akiamini ndiyo njia pekee ya kuisaidia timu ifanye vizuri.

Dua na sala hizo Lugola anaamini zitafika kwa Mwenyezi Mungu ili kuipa suluhuhisho Stars iweze kufanya vizuri katika mechi ijayo dhidi ya Uganda itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

LihatTutupKomentar