HUYU HAPA MBADALA WA MANJI YANGA



Baadhi ya wanachama wa Yanga wamejitokeza na kumtaka Abbas Tarimba kugombea nafasi ya uenyekiti ndani ya klabu hiyo.

Wanachama hao baadhi wamesema Tarimba ndiye mtu pekee ambaye anastahili kuchukua nafasi ya Yusuf Manji endapo hatojitokeza kugombea nafasi hiyo.

Tarimba ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Yanga na kuanzisha suala la kuibadili klabu hiyo kuwa kampuni anapigiwa upatu wa kugombea nafasi hiyo.

Tayari Shirikisho la Soka Tanzania limeshapanga tarehe ya kufanyika uchaguzi huo ambao utakuwa Januari 1 2019.

Uchaguzi huo utasimamiwa na Kamati za Uchaguzi mbili ambazo ni ile ya TFF kwa mujibu wa BMT na Yanga wenyewe.

LihatTutupKomentar