Baada ya wachezaji wa wawili wa timu ya Yanga kugoma kusaifir na timu kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kusema wanakabiliwa na matatizo na si madai ya mishahara, imeelezwa.
Kwa mujibu wa Meneja wa timu, Nadir Haroub 'Cannavaro, imeelezwa amesema wachezaji hao ambao ni Beno Kakolanya na Kelvin Yondani hawaidai chochote Yanga mpaka sasa.
Cannavaro ameeleza kuwa wawili hao wamekubwa na matatizo kadhaa jambo ambalo limepelekea wasisafiri kuelekea Shinyanga mpaka wakabakia jijini Dar es Salaam.
Licha ya Cannavaro kueleza hayo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, majira ya jana mchana alisema jambo togauti kwa kukiri kuwa wachezaji hao wanaidai timu.
Lakini baadaye Cannaro naye akajaa na kauli nyingine ambayo inaleta mkanganyiko baina yao wawili juu ya Beno na Yondani kusalia Dar es Salaam.