HAWA HAPA KUTUA SIMBA USAJIRI DIRISHA DOGO



Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umeanza mchakato wa kuwania saini za wachezaji wawili kutoka Gor Mahia FC kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems anazihitaji.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza wachezaji Philemon Otien na Ephrem Guikan ndiyo wanaowaniwa kwa ajili ya usajili pindi dirisha dogo litakapofungulowa Novemba 15 2018.

Wachezaji hao wawili wanacheza nafasi tofauti ambapo Guikan anakipiga katika nafasi ya ushambuliaji huku Otien akicheza nafasi ya kiungo.

Usajili huo umekuwa pendekezo la Aussems ambaye amedhamiria kukijenga kikosi cha Simba vema akiwa na malengo ya kukifikisha mbali pia kwenye mashindano ya kimataifa.

Mbali na wachezaji hao, ilielezwa pia Simba wataendelea kufukuzia saini ya Francis Kahata ambaye walianza kumnyemelea tangu msimu uliopita huku ikielezwa ana majina mengine pia ambayo atahitaji yasajiliwe.

LihatTutupKomentar