WAWA AFUNGUKA KUHUSU ERASTO NYONI

Beki wa kati wa timu ya Simba raia wa Ivory Coast Pascal Wawa, ambaye alianza soka  katika klabu ya ASEC Mimosas amefunguka kuwa mpango wa kumrejesha Stars beki kiraka Erasto Nyoni ulianza kwenye mazoezi .

Nyoni ambaye alitemwa mwazoni katika kikosi cha Stars kwa kile kilichodaiwa kuwa ni utomvu wa nidhamu na kushindwa kuitwa kwenye kikosi kilichowavaa Cape Verde ugenini ,alikuwa uwanjani wakati Stars ikiwafunga mabao 2-0 Cape Verde uwanja wa Taifa.

"Nyoni ni mchezaji mzuri nimekuwa naye karibu, nimemshauri vitu vingi hasa katika kuzingatia mazoezi hali ambayo imemfanya awe bora zaidi na kuweza kupata namba kwenye timu yetu pamoja na timu ya Taifa.

"Nimekuwa nikimpa ushauri Nyoni  hasa kuweza kujiweka vizuri  kwa kuzingatia nidhamu na kujituma hali ambayo inambadilisha kila leo hivyo,nimekuwa nikifanya kwa wachezaji wengi na kwa yule ambaye atafuata kile ambacho ninamwambia atafika mbali"alisema .

LihatTutupKomentar