UHOLANZI WAMFUNGIA BEKI WAO KISA HIKI HAPA



Beki wa timu ya taifa ya Uholanzi, upande wa vijana chini ya miaka 20, Jordan Teze amefungiwa kucheza michezo ya kimataifa baada ya kumtemea mchezaji wa Ujerumani.

Teze alimtemea mate Salih Ozcan wakati timu hizo zilizokutana na kutoka kwa safe ya bao 1-1.

Suala hilo, limeanza kulinganishwa na like la beki wa zamani wa timu hiyo ya taifa, Frank Rijkaard kumtemea mate Rudi Voller wa Ujerumani wakati wa Kombe la Dunia mwaka 1990.

Shirikisho la Soka la Uholanzi, limesisitiza kwamba ni mambo muhimu sana kuwa na nidhamu sahihi kwa ajili ya kutengeneza ubora ambao Uholanzi unautaka.

LihatTutupKomentar