SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA. MTUNZI;RAJA SAIDY. WHATSAPP;0756920739

SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.

SEHEMU YA NNE.

ILIPOISHIA...............

"we si unaenda duniani unatakiwa uchague mtu kwenye familia yako ambaye atakuja huku ili uweze kuwasaidia wanao,na ukisema aje mke wako haiwezekani mke wangu ananguvu sana na yeye ndiye anayewaleta huku sa uchague kati ya nadya na caro nani aje huku ili wewe uweze kupata nafasi ya kwenda huko duniani kupambana na mama yao kisha ukirudi kuzimu na utakaye kuwa umemchagua na yeye atarudi duniani"
je nini kitaendelea...........

ENDELEA NAYO.........

***************************

"Mungu nisaidia mimi nadya,ona navyoteseka mungu niangalie kwa jicho la tatu mungu,nipo chini yako mungu naomba mama yangu ashindwe kwa chochote anachokifanya juu yangu,mungu mchome moto utakaoenda kuangamiza nguvu zake za giza,nguvu za kichawi,na nguvu zote za kishetani AMINA"
  Nilifanya ibada ya muda mfupi huku bado nikiwa pale chini,ghafla sikuamini baada ya kujisikia naanza kupata nguvu mpya na kunifanya  niweze kusimama upya,niligeuka upande wa pili kwa masikitiko makubwa,nilitahamaki na kushangaa baada ya kumkuta mdogo wangu caro bado akiwa pale pale chini huku akiwa amepoteza fahamu.
    Nilipiga hatua chache za haraka haraka huku mwilini mwangu nikijisikia ni mwenye nguvu za kufanya chochote kile,nilifanikiwa kufika mpaka mahali ambapo mdogo amepoteza fahamu kisha nikaanza kumuamsha kwa lengo la kurudisha fahamu zake,
"caro,caro,caro,caro mdogo amka amka caro,mimi ni mzima angalia caro mimi dada yako nimesimama amka basi"
  cha ajabu baada ya kuwa nimejitambulisha kama dada yake caro,caro aliweza kunisikia vyema na kuitikia wito wangu kisha akaanza kuamka kana kwamba alikua kwenye usingizi mzito na wa maajabu.
"dada nadya nipo wapi na hapa nafanya nini?"
"mdogo wangu caro,ulikuwa umepoteza fahamu baada ya kuwa nimekupa taarifa za msiba wa baba......."
"Dada nadya mama yuko wapi??"
   Caro alinitupia swali lile lililonifanya nikimbie haraka kuelekea chumbani kwa mama huku nikimuacha caro akiwa bado ni mtu aliyeshindwa kurudisha kumbukumbu za tukio liliyopita kabla ajapoteza fahamu.
     Nikiwa tayari nimefanikiwa kufika chumbani kwa mama ghafla mwili wangu ulianza kutetemeka huku kijasho chembamba kikiendelea kunitoka kwa nilichokiona.

**********************
"mkuu sitakubali mwanangu yeyote aje huku kuzimu apate mateso kama nayoyapata hivi sasa na sidhani kama kuna mwanangu yeyote anaweza kuishi maisha ya huku hata kidogo,tafadhali mkuu naomba sharti jingine tafadhali tofauti na hilo la kuchagua mwanangu kuja huku"
"bwana thomas sina kingine cha kukusaidia kuhusu wanao akiwa ni caro na nadya.kama umeshindwa kufanya shart hilo basi,maana nadhani ukifanya hivyo itakuwa njia moja wapo ya kuwalaghai mizimu maana wana idadi ya kila anayejiunga humu ila hawana idadi kila anayejiondoa humu maana wanachojua wao ni vigumu kutoroka kuzimu maana tayari we duniani ni mfu na ukienda unaishi kama nafsi,hiyo ndo sababu kuu inayowafanya wawe na idadi ya wanaojiunga na pia kinachofanya ujiunge kuzimu ni dhabi zako mimi sikukuleta bwana thomas ulitenda dhabi mwenyewe duniani yamekukuta yaliyokukuta na mke wako tunamsubili kwa hamu kama wewe tulivyokuwa tunakusubili"
"najua mkuu yote ni makosa yangu ila huu sio muda husika wa kujilaumu ila nachotaka niwasaidie wanangu wasiweze kuja huku kama mimi, huku kuna shida wataweza kulaumu uzao wangu watamuudhi mungu kwa kusema heli nisinge waleta dunia na hii itakuwa laana ya uzao wangu ujao utakaotoka kwa wanangu waliobakia"
"basi sawa nimekuelewa bwana thomas ila shart ni moja nalokupa huko duniani,uende ukawasaidie wanao ila kitu kimoja,mama yao ananguvu sana na anaouwezo wa kukurudisha huku naomba ufanye kitu kimoja jitahidi asingundue kuwa umerudi duniani kama mzimu hakikisha hilo,safari njema".
"ahsante sana mkuu naenda kuwasaidia wanangu mkuu kisha nitarejea"
"sawa safari njema.

************************
     Baba yake thomas abaye ni babu yake nadya aliaanza kujiaandaa kwa safari ya kuelekea mjini kwa ajili ya kumuuwa mama nadya kwa sababu ya kumuuwa mwanae bila kosa,kabla ajaanza safari alianza kuongea mwenyewe Mithili ya kichaa,

"nafunga safari ngoja nielekee mjini kupambana na huyo mama nadya lazima nimuuwe haiwezekani anamuuwa mwanangu thomas,amemkosea nini,amemfanyia nini yani amevunja mila za kwetu kabisa anashindwa kuishi na mwanangu kwa miaka tuliyokubaliana kuwa atadumu kwenye ndoa,sasa basi safari yangu inafikia kwenye nyumba ya mwanangu sa ngoja tuone kama ataweza uganga wangu"
"mama thomas njoo mke wangu unisindikize naelekea mjini kwa mwanangu kumuenzi maana hata msibani hatujaalikwa,mwili wa mwanetu hatujauona"
"unasemaje baba thomas,thomas wangu amekufa???"
"Ndio"
"we umejuaje???!"
"mizimu imeniambia we unajua hapa kijijini asilimia kubwa taarifa nyingi tunapokea kutoka kwenye mizimu vita ya kikabila kila kitu,muda wa njaa,kiangazi muda gani kitakuepo,we si unajua kila kitu ni mizimu"
"mama weeee weeeeee  mwanagu mwanangu thomas uwiiiiiiii mme wangu mbona hukuniambia toka zamani.........?"
""mke wangu naomba ukae kimya ndio nilikuwa sitaki kukupa taarifa hizi utakorofisha mizimu"

    mama thomas alimtupia swali mumewe huku akiendelea kufuta machozi
"nani amemuuwa mme wangu???"
"mke wake"
"eti nani mme wangu leo nauwa mtu twende huko huko mjini kitaeleweka lazima ale nyama ya mwanangu haiwezekani"
JE  MAMA NADYA ATAWEZA KUPAMABANA NA WATU HAWA WATANO; MZIMU WA MME WAKE,BABU YAKE NA NADYA ,BIBI YAKE NA NADYA,CARO NA NADYA MWENYEWE USKOSE SEHEMU IJAYO...............

LihatTutupKomentar