SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA. MTUNZI;RAJA SAIDY. WHATSAPP;0756920739.

ASIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.

SEHEMU YA TATU

ILIPOISHIA...............

"mungu najua nilikukosea,mungu najua mi nimkosefu muda wote ila wanasema  mungu hamtupi mja wake nadhani hata mimi hivyo hivyo uwezi nitupa,naweka imani yangu yote kwako naomba uniokoe katika adhabu hii katika kifungu hichi cha dhabi,ushetani,uchawi na nguvu za giza,mungu nakutegemea wewe maana wewe ndo msaada wangu katika maisha yangu AMEN"
   Nikiwa nimemaliza maombi ghafla......................
JE NINI KITAENDELEA .......................

ENDELEA NAYO......................

Nilianza kujisikia mwepesi kisha nikasimama kama kawaida,nakuelekea nje.nikiwa tayari niko nje ya chumba cha mama,nilimkuta mama akiwa anaanika nguo huku mdogo wangu caro akiwa ameshika kiuno chake huku akiendelea kuangaza wapi nilipo aniletee simu,
"we caro nakuambia unipe hiyo simu hutaki ganda nayo sasa tuone kama utampata huyo nadya wako"

mama alimwambia caro,huku akiendelea kuanika nguo,kabla mama hajaniona caro aliniita kwa furaha huku moyoni mwangu nikiwa tayari nimeshajenga chuki juu ya mama yangu mzazi,jambo lililofanya nikae kimya muda wote huku nikiendelea kufikiria nifanye nini cha kumuuwa mama ili apotee duniani.

"dada nadya,ulikuwa wapi simu yako kutoka ofisini  ilikuwa inaita"
caro alizungumza huku akininyooshea mkono kwa ajili ya kunikabidhi simu,wakati akiwa anaendelea na zoezi lile
ghafla mama alianza kutetemeka huku akigeuka kwa kunishangaa na kushindwa kuamini kuwa ni mimi au mzimu wangu.
   Mama alitupa ndoo iliyokuwa na baadhi ya nguo zilizokuwa tayari kwa ajili ya kuanikwa kisha akaingia ndani bila ya kuzungumza na mtu yeyote,kitendo hicho kilimshangaza caro kisha akaniuliza,
"dada kuna nini kati yako na mama halafu jana niliota ndoto mama amekufanya dondocha,baada ya hapo mungu akakusaidia ukatoka kwenye huo udondocha,kisha mama akafanya mpango akakuuwa.ndoto mbaya dada nilitaka nikuambie asubuhi lakini nikawa na usingizi,nadhani hii ilitokana na kutokusali kwetu"
"caro unasemaje mimi nikafa mimi,mimi hamna sio kweli"

nilianza kuongea maneno mengi yasiyokuwa na maana mithili ya mtu aliyeanza kuchanganyikiwa kitendo kile kilimfanya caro aanze kutoa machozi huku akiendelea kuzungumza.

"baba,baba amka dada nadya amechanganyikiwa,mama njoo mama njoo njoo mama nadya dada yangu dada yangu"
      caro aliendelea kuzidisha kelele hasa pale alivyoona nadya anaanza kutoa mapovu mdomoni na hali hii imeanza kumkumba  nadya baada ya mama yake kuingia ndani na kuanza kumchezea kwa nia ya kummaliza.
     baaada ya kuwa caro ameona hali ile imezidi kumtawala dada yake aliingia chumbani mwa mama yake kwa fujo na kumkuta mama yake akiwa uchi wa mnyama huku akiwa amewasha mshumaa pia akiendelea kuuzunguka, caro akiwa amesimama na kushangaa maajabu yale,alianza kusikia maneno aliyokuwa anazungumza mama yake kipindi alicho kuwa anazunguka mchumaa,

"nadya kufa nadya kufa,kufa nataka nyama yako njoo njoo kuzimu"

  kitendo kile kilimfanya caro amuulize mama yake huku akihema kwa shida na kushindwa kuamini kama mama yake ni mchawi tena asiyekuwa na huruma,

"ma..........ma..........kumbe...wewe ni mchawi si ndio mama!!!!! unataka kumuuwa nadya kakukosea nini we mama si unijibu ntakuuwa na mimi,baba njoo tumuuwe mama anataka kumuuwa nandya njoo"
  caro alianza kuongea kwa ujasiri mkubwa bila ya kujua kuwa baba yake kaisha fariki,mama yake aliendelea kuwanga kama kawaida kana kwamba hakusikia mwanae caro akiongea jambo lolote,kitendo hicho kilimfanya caro kupiga magoti chini huku akilia kwa uchungu,na kumuomba mungu amuepushe na dhabi atakayoenda kuitenda muda sio mrefu,caro aliomba kimya kimya bila mtu yeyote kusikia,
"mungu naomba unisamehe kwa nachoenda kukifanya"
Baada ya kuwa  caro ameomba kwa muda mfupi alitoka nje na kuelekea jikoni kufuata kisu,alipita nje na kumkuta dada yake nadya bado akiendelea kushika tumbo huku akilia,
"Caro,mama ni mchawi amemuuwa baba,na wewe atakuuwa"
taarifa ile iliyotoka kwa nadya ilimfikia caro na kumfanya asimame kwa mshangao kisha akadondoka chini na kupoteza fahamu.

*******************
"mkuu naomba ruhusa niende duniani kuwaokoa wanangu angalia mama yao alivyomkatili kitendo cha kuambiwa kuwa endapo akimaliza familia yake yote atapandishwa cheo hapo ndipo walipokosea maana amekuwa mkatili sana ameniuwa mimi,na usipo nipa ruhusa pia hivyo hivyo atawauwa wanangu naomba ruhusu mkuu sitaki watoto wangu waje hapa nilipo najua mateso ya kuzimu ni makali ni makali sana ni vipi wanangu watoke kula nyama za ng'ombe huko duniani waje huku waanze kula nyama za binadamu na damu ya binadamu na wakati njia ya kuwaepusha kuja huku ipo,nakuomba mkuu nadya wangu atakufa,caro wangu atakufa nakuomba"
"sawa nimekupa ruhusa ila unatakiwa uchague kati ya familia yako nani aje huku kuziba nafasi yako"
"unamaana gani mkuu????"
"we si unaenda duniani unatakiwa uchague mtu kwenye familia yako ambaye atakuja huku ili uweze kuwasaidia wanao,na ukisema aje mke wako haiwezekani mke wangu ananguvu sana na yeye ndiye anayewaleta huku sa uchague kati ya nadya na caro nani aje huku ili wewe uweze kupata nafasi ya kwenda huko duniani kupambana na mama yao kisha ukirudi kuzimu na utakaye kuwa umemchagua na yeye atarudi duniani"
je nini kitaendelea...........................

LihatTutupKomentar