SAID NDEMLA AFUNGUKA MAKUBWA SIMBA



Baada ya kuonekana akifanya mazoezi na timu ya Simba B, kiungo Said Ndemla  amefunguka kuwa ameamua kujiongezea dozi ya mazoezi ili kuwa fiti zaidi.

Ndemla amekuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa siku tofauti na wachezaji wengine amekuwa akijifua na kikosi cha Simba B asubuhi uwanja wa Kinesi chini ya kocha Nico Kiondo , jioni amekuwa akijiunga na timu ya wakubwa Uwanja wa Boko Veterani .

"Nimekuwa nikifanya mazoezi na timu ndogo ya Simba pale Kinesi sio tatizo ni jambo la kawaida, huku kwenye timu yangu nako nafanya mazoezi kama kawaida bila shida yoyote na lengo ni kujiweka fiti.

"Na hii inanisaidia kuwa vizuri zaidi kama unavyofahamu soka siku zote ushindani ni mkubwa na unahitaji kuwa imara nyakati zote bila kuzubaa"alisema .

LihatTutupKomentar