REAL MADRID WAACHANA NA JULLEN LOPETEGUI

Baada ya Real Madrid kumfukuza kocha mkuu wa klabu hiyo Jullen LOPETEGUI  baada ya matokeo mabovu ya timu hiyo msimu huu 2018/2019  .
::
::
Kocha huyo ambaye ameiongoza Real Madrid katika mechi 14 na kushinda 6 ,droo mbili na kupoteza mechi 6 miongoni mwa mechi aliyoipoteza ni kipigo cha goli 5-1 dhidi ya Barcelona katika Elclasico .
::
::
Ikumbukwe pia   Kocha huyo wa zamani wa Spain alifukuzwa na  chama cha soka cha Spain siku chache tu kabla ya kombe la dunia baada ya taarifa kusambaa kuwa amejiunga na Real Madrid bila kuwapa taarifa viongozi wa chama cha soka Spain.
::
::
Taarifa  Kutoka chama cha soka cha spain zinasema kuwa Madrid wana wiki mbili kuchagua kocha mkuu wa timu hiyo kwa mujibu wa sheria namba 160 katika Sheria za chama hicho ambayo inasema ikiwa timu itakufukuza kocha wake huku ligi ikiendelea ni lazima wachague kocha mkuu ndani ya wiki mbili ambaye ana linseni ya ukocha ..
::
::
Pia ikiwa Madrid atashindwa kufanya ivo ndani ya wiki mbili ataazibiwa kwa mujibu wa sheria ya chama hicho.

Kwa sasa Antonio Conte ndiye anayepigiwa upatu zaidi kuchukua nafasi ya lopetegui aliyefukuzwa kuamkia Leo.

Kwa sasa nafasi hiyo inashikiliwa na mchezaji wa zamani klabu hiyo Santiago Solari  aliyekuwa kocha wa timu ya akiba  ya real Madrid ..!!
Huenda Madrid wakaamua kumuajiri moja kwa moja kocha huyo ikiwa watashindwa kumpata mbadala wa lopetegui.

LihatTutupKomentar