MWINYI ZAHERA AFUNGUKA HAYA

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwa sasa ameelekeza nguvu dhidi ya Zimbabwe keshokutwa.

DRC Congo itaivaa Zimbabwe kwao Harare kuwania kucheza Afcon na Zahera ni kocha msaidizi wa Congo.

Zahera ameiambia SALEHJEMBE atarejea na kujiunga na Yanga siku moja baada ya mechi hiyo tayari kuendelea na maandalizi ya ligi.

"Kwa sasa tuko Harare, tunasubiri mechi baada ya maandalizi. Nguvu yote hapa lakini baada ya hapo narudi kuendelea kupambana," alisema.

Kocha huyo Mkongo ameifanya Yanga kuwa imara tofauti na ilivyokuwa ikionekana hapo awali hasa hofu kwa mashabiki kwamba kikosi chao kiko katika hali mbaya sana.

LihatTutupKomentar