MJUE NA KUMFAHAMU KITWANA MANARA ALIYEWIKA KAMA GOLIKIPA NA MSHAMBULIAJI HATARI TANZANIA

MJUE NA KUMFAHAMU KITWANA MANARA ALIYEWIKA KAMA GOLIKIPA NA MSHAMBULIAJI HATARI TANZANIA

Wasifu wa Kitwana Manara

-Alianza kama golikipa akikaa langoni kuanzia mwaka 1959 hadi 1968.

-Alidakia timu za Cosmopolitan ya Dar es Salaam na kuwa mabingwa wa Ligi ya Dar Es Salaam mwaka 1964. Hiyo ilikuwa kabla ya kuanzishwa kwa ligi daraja la kwanza Tanzania iliyoshirikisha timu za bara na Zanzibar iliyoanza rasmi mwaka 1965.

-Mwaka 1965 alitimkia  Kenya kuidakia timu ya Feisal FC ya jijini Mombasa na kuisaidia kushinda ubingwa wa Kenya.

-Kwa kwenda Kenya, Kitwana akawa mwanasoka wa kwanza wa Tanzania kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

-Mwaka 1966 alirudi nchini na kujiunga na klabu ya TPC ya mkoani Kilimanjaro iliyokuwa inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania ( sasa inaitwa ligi kuu Tanzania bara )

-Mwaka 1967 alirudi timu yake ya zamani Cosmopolitan na kuisaia kushinda ubingwa wa  ligi daraja kwanza Tanzania.

-Mwaka 1968 akajiunga na klabu ya Yanga na kuisaidia kushinda ubingwa wa Tanzania kwa mara ya kwanza akiibuka kinara langoni kwa ustadi wake .

-Mwaka 1969 akaachana na ukipa nakuanza kucheza kama mshambuliaji wa kati. Akaisaidia Yanga kushinda ubingwa wa Tanzania mara nne mfululizo hadi 1972 akisimama kama muhimili katika upachikaji magoli na kuwashangaza wengi waliyozoea kumuona langoni.

-Alipokuwa kipa aliidakia timu ya taifa, alipokuwa mshambuliaji, aliichezea timu ya taifa ‘ Taifa Stars ‘. Hii ni rekodi yake ya pekee ambayo haijavunjwa mpaka sasa.

-Alistaafu timu ya taifa mwaka 1976 baada ya kufukuzwa(yeye na wenzake wengi)  Yanga. Yanga ilivurunda sana mwaka huo na kuamua kusuka upya kikosi chao.

-Alicheza kama mshambuliaji hadi mwaka  1986 alipostaafu soka rasmi.

LihatTutupKomentar