IGP SIRRO AMELIANIKA GARI LINALOAMINIKA KUTUMIKA KUMTEKA MO DEWJI




Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simoni Sirro amezungumzia tukio la kutkwa kwa mfanyabiashara na Mwekezaji wa Simba,Mohamed Dewij ‘Mo’, ikiwa pamoja na kuelezea hatua za upelelezi wao ambapo wameinyesha gari lililomteka.

Mbali na hilo Sirro amesema watu waliomteka Mo inaonekana walitokea nje ya mpaka wa Tanzania,hivyo kwa kushirikiana na Interpo wameshaenda nchi husika kujilidhisha zaidi.

“Gari hilo baada ya kufanya tukio la utekaji kwa mujibu wa CCTV tumebaini lilipitia barabara ya Haile Selassie,Ally Hassan Mwinyi,Kimweri, Maandazi, Mwai na Mwai Kibaki.

“Baadae lilipotea kwenye eneo la Mlalakuwa karibu na mzunguko wa Kawe, hivyo tunaamini kuwa wapo watu walioliona gari hilo likipita.

Kwa kua ni barabarani tunaamini watu wataendelea kutusaidi kuonyesha lilipoelekea kwa kua tayari kulikuwa kumepambambazuka.

Hivyo tunawaomba mashuhuda hasa watu wenye CCTV zao watusaidie kuangalia katika maeneo ya Msasani ambapo pengine hatujazitambua na kuzichunguza,” alisema Sirro.

LihatTutupKomentar