ALLIANCE FC WAAPA KUWAGALAGAZA YANGA

Ofisa habari wa timu ya Alliance School, Jacson Mwafulango amesema kuwa wamepata majibu ya timu ya Yanga ambao watacheza nao October 20 katika uwanja wa taifa.

Mwafulango amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo kwenye ligi kuu na mwendo wao ni wa tahadhari kubwa na  amewataka wapinzani wasiwabeze kwani nia yao ni kuleta ushindani.

"Timu yetu ipo vizuri na tutapata matokeo katika mchezo wetu dhidi ya Yanga ,tumewafuatilia vizuri , tunawajua na tunawaheshimu hivyo majibu yao tunayo kwa kuwa hatuna hofu.

"Tutawafundisha namna mpira unavyochezwa kwani sisi ni taasisi ambayo vijana wetu wanafundishwa mpira wa darasani , wamekaa pamoja kwa muda mrefu hivyo tutawashangaza wengi"alisema

LihatTutupKomentar