TFF YATANGAZA SIKU ZA MAOMBOLEZO KWA WALIO PATA AJARI MV NYERERE


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewaagiza Wanachama wake kuhakikisha katika mechi zote za Ligi kunakuwa na dakika moja ya ukimya na kufunga vitambaa vyeusi kuomboleza waliofariki kwenye ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichozama kati ya Ukara na Bogorara, Ukerewe.
Utaratibu huo utafanyika katika mechi zote mpaka kipindi cha maombolezo yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli kitakapomalizika.
Tayari utaratibu huo umeanza kwenye mchezo wa Ijumaa kati ya KMC na Stand United uliochezwa Uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam.
Mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi,Amina.
LihatTutupKomentar