TFF WAZUNGUMZIA KUHUSU MTIBWA KUTO PEWA HELA ZA UBINGWA WA FA

Baada ya klabu ya Mtibwa Sugar kulalamikia kutopewa fedha zake za mshindi wa Kombe la FA, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limeibuka na kusema Mtibwa hawawezi kuzungumzia suala hilo.
Kwa mujibu wa Radio One, Mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi, amesema kwa namna anavyowafahamu Mtibwa Sugar hawawezi wakatoa kauli kama hiyo.
Madadi ameeleza kuwa Mtibwa wamekuwa ni watu wastaarabu hivyo haamini kama wanaweza kuzungumza kwenye vyombo vya habari wakilalamikia kuwa hawajapewa fedha zao.
Aidha, Madadi ameeleza kuwa kwa sasa hatakuwa na kuzungumza zaidi na badala yake watakuja na tamko lao kuhusiana na fedha hizo siku za usoni.
Mtibwa inadai kitita cha fedha ambazo ni shilingi za kitanzania, milioni 50 baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United Juni 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

LihatTutupKomentar