SIMBA YAWAVURUGA WAZANZIBARI


Wakati uongozi wa Simba ukiweka hadharani kuwa kikosi chao hakitosafiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi maalum dhidi ya Yanga, unaambiwa mashabiki wengi visiwani humo wamepigwa na butwaa.

Mashabiki hao tangu majira ya asubuhi walikusanyika maeneo mbalimbali visiwani humo wakiwasubiria kwa hamu wachezaji wa timu hiyo baada ya kutowasili kwa muda mrefu lakini hawakuambilia kitu.

Uwepo wa nyota wapya kama Meddie Kagere, Clatous Chama, uliwaoa jeuri ya mashabiki hao kuisubiria timu ya Simba baada ya kupata taarifa kuwa watawasili kujiandaa na mechi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Licha ya kusubiria na muda ukizidi kwenda, walishangaa kuona hakuna chochote kinachoendelea juu ya kuwasili kwao hadi majira ya jioni kabla Simba hawajatoa taarifa rasmi.

Lakini baadaye mida ya jioni uongozi wa Simba kupitia kwa Msemaji wake, Haji Manara, uliibuka na kusema umesitisha mipango hiyo ili kutowapa uchovu wachezaji wake na kwa maana hiyo kikosi kitaendelea na mazoezi kikiwa Dar es Salaam.

LihatTutupKomentar