SIMBA YAENDELEA NA MAZOEZI LEO

Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkana uliopo jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi za Ligi Kuu Bara.

Kikosi hicho kimeongezeka baada ya wachezaji waliokuwa wamechelewa kujiunga na kambi ya Taifa Stars kisha kuondolewa, wameanza mazoezi na wenzao tayari kukabiliana na Ndanda huko Mtwara.

Ndanda itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wao wa Nangwanda Sijaona Septemba 15 2018.

Wakati Simba wakijiandaa, Ndanda FC nao wako katika maandalizi moto wakijiandaa kujibu mapigo ya mnyama ambaye amedhamiria kuuchukua ubingwa wa ligi kwa miaka mitano mfululizo.

LihatTutupKomentar