PEP GUARDIOLA AMKUBARI MOURINHO

TANGU Manchester United wapate kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Tottenham katika Uwanja wa Old Trafford, mambo yanaonekana kwenda ndivyo sivyo.

Baada ya kichapo hicho, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, alionekana kuwaambia waandishi wa habari kuwa anahitaji heshima, sababu ni kocha pekee aliyeshinda mataji matatu ndani ya Ligi Kuu England kuliko wengine 19 waliopo.

Lakini pia Mourinho aliendelea kwa kusema kuwa yeye ni mmoja wa makocha bora duniani, licha ya timu yake kufanya vibaya hivi sasa.

“Nimeshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England, mengi zaidi ya wengi wote 19 waliopo hapa.

“Nimeshinda mataji katika ligi tatu tofauti, hakuna kocha aliyewahi kufanya hivyo zaidi yangu, nahitaji heshima,” alisema Mourinho.

Baada ya kauli hizo, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema kuwa wanaomsema vibaya Mourinho hawajielewi.

Guardiola alisema bado ni mapema huwezi kuwatoa Manchester United katika mbio za ubingwa kwa kuchezwa michezo mitatu tu ya Ligi Kuu.

“Mourinho ni kocha mkubwa, hilo silipingi, nashangaa wanaomsema ovyo na kusahau kuwa ni michezo mitatu imechezwa hadi sasa, nafasi ya kutwaa taji bado wanayo,” alisema Guardiola.

Manchester United wameshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Leicester City na kufungwa miwili mfululizo hivi karibuni dhidi ya Brighton na Tottenham.

LihatTutupKomentar