MEDDIE KAGERE AFUNGUKA KUHUSU SIMBA

Akiendelea na kasi yake mabao katika Ligi Kuu Bara , mshambuliaji tegemeo hivi sasa wa Simba Mnyarwanda, Meddie Kagere ametaja siri ya mabao yake.
Mnyarwanda huyo hadi sasa tayari ameifungia timu yake mabao tisa tangu ajiunge nayo akitokea Gor Mahia katika usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Katika mabao hayo tisa, matatu kafunga kwenye ligi, Kombe la Kagame manne na mengine mawili katika michezo ya kirafiki ambayo imecheza., Kagere alisema maelekezo anayoyapata kutoka kwa kocha wake Mbelgiji, Patrick Aussems ndiyo chachu ya yeye kufunga mabao katika timu hiyo.
Kagere alisema, alitaka kingine ni ushirikiano mzuri anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake katika kufanikisha matokeo mazuri na mwisho wa mechi wanaibuka na pointi tatu.
“Kama wachezaji kitu tulichokubaliana kwa pamoja ni kuwapa furaha mashabiki wetu ambayo wanaipata kutokana na matokeo mazuri tunayowapa, mimi hakika mbinu za Mbelgiji zinanisaidia sana.
“Mfano mimi ni mshambuliaji ni lazima nitimize majukumu yangu ya kufunga mabao kwa kutumia kila nafasi ninayoipata, viungo wao ni kuchezesha timu kwa kutupa pasi za kufunga mabao na mabeki kuzuia hatari zote zinazotokea golini kwetu.
“Hivyo, hiyo ndiyo siri pekee ya mimi kuniona nikifunga mabao Simba na kikubwa tunataka kuwaona mashabiki wetu wakipata furaha kila wakijitokeza uwanjani kutusapoti,”alisema Kagere.

LihatTutupKomentar