WILIANI MAISHA YA CHELSEA NAYAPENDA SANA

LONDON, England
WINGA wa Brazil, Willian, ameibuka na kuweka wazi kuwa, hana matatizo yoyote na uongozi wa klabu yake ya Chelsea.
Kiungo huyu aliyeng’ara na Brazil kwenye Kombe la Dunia, alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, ana furaha kubaki London na hana mpango wa kuondoka kwa sasa.
“Sikweli kama sina furaha. Hapa Chelsea ni nyumbani kwangu. Nina amani na ninapenda kuendelea kubaki London,” alisema Willian.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi za kuonyesha kuwa Willian anakaribia kuondoka Chelsea na kutimkia Real Madrid au Manchester United.
Inaelezwa kuwa, Willian anataka kuondoka Chelsea na kwenda mahali atakapopata nafasi ya kucheza mara kwa mara
LihatTutupKomentar