VILABU VYA SIMBA NA YANGA VINAKOSEA HAPA.

Na
MOSES FRANCIS+255715878724

Hebu fumba macho sekunde 30. Litafakari goli alilofungwa Aishi Manula na Kevin Kongwe wa Mtibwa Sugar katika pambano la ngao ya jamii. Ni goli la kawaida tu. Paschal Wawa na mwenzake Erasto Nyoni hawakuwa na mawasiliano mazuri. Kongwa alipokea pasi akiwa hajakabwa nje kidogo na penati boksi akapiga na akafunga. Ni goli la kawaida tu. Ni aina ya magoli ambayo mashabiki wa Simba na Yanga pamoja na viongozi wao huwa yanawakuna hasa katika mechi muhimu. Mfano endapo Simba  ikicheza mechi muhimu dhidi ya Mbao Fc na ikafungwa goli la namna ile. Utawasikia wakisema mwakani tunamtaka huyo lazima asajiliwe. 

Kuna washambuliaji wengi sana nchi hii wamekula pesa za Simba na Yanga kwasababu wamefanya vizuri mechi moja tu. Huwa wanazifunga timu hizi magoli ya kawaida tu lakini mashabiki pamoja na viongozi wa timu hizi huwa wanayapa hadhi magoli hayo kwa kuyapa thamani kubwa. Magoli kama ya Kelvin Kongwe dhidi ya Simba ni aina ya magoli ambayo yanafungwa sana hata katika mechi dhidi ya Maji Maji na Stand United. Magoli hayo hubakia vile vile kwa kutokupewa hadhi kama yale ambayo Simba na Yanga wanafungwa kwasababu timu kama Maji Maji au Stand United ni timu ambazo hawazishabikii.
Kwa mfano katika pambano la ligi kuu msimu uliopita mechi ya Simba na Lipuli pale Iringa. Ni mechi ambayo Adam Salamba alijikatia tiketi ya kwenda Simba. Salamba alikuwa anakimbia na mpira kuelekea katika lango la Simba bahati mbaya beki wa Simba Mlipili aliteleza na ndipo Salamba alipopata mwanya wa kufinya na akawa amemtungua Aishi Manula. Ni goli la kawaida tu. Lakini kwa jinsi tulivyojijengea mazoea kwa kukipa thaman kitu ambacho ni cha kawaida na kuonekana ni kikubwa au cha ajabu basi ndio ikawa ni tiketi ya Salamba kutua Simba mwaka huu. Yanga pia waliwahi kumsajili Busungu kutoka Mgambo Jkt ya 
Tanga nasikia aliwasumbua sana katika mechi yao ya kwanza pale Mkwakwani. Haya ni maisha ambayo hata washambuliaji wa timu ndogo wanajua kuwa ukizisumbua Simba au Yanga hasa katika mechi muhimu basi kuna uwezekano msimu ujao wakasajiliwa na timu hizi za kariakoo. Marcel Kaheza ndiye mshambuliaji bora msimu uliopita ukimweka pembeni Emmanuel Okwi. Kaheza na mwenzake Bocco walimaliza ligi wote wakiwa na magoli 12. Kaheza anastahili kuchezea Simba kwa sasa kutokana na rekodi aliyonaipata msimu uliopita. Kevin Kongwe endapo angeifunga Simba goli lile ligi kuu huenda msimu ujao angesajiliwa na Simba. 

LihatTutupKomentar