SIMBA, MTIBWA SUGAR HISTORIA ITAWAHUKUMU.

Na MOSES FRANCIS
+255715878724

Watanzania tulio  wengi tunaishi kwa mazoea. Ndio tunaishi kwa mazoea. Mtanzania mwenzangu anataka asome, apate kazi, aajiriwe, apate pesa baadae asitaafu. Mtanzania mwenzangu ameyaishi maisha haya kwa muda mrefu sana. Maisha ambayo yamejengea kiburi na hali ya mazoea. Kuna kundi kubwa sana la wanafunzi wahitimu vyuo vikuu kwa sasa wanalalamika kuhusu ajira. Rais wangu Magufuli sasa hivi amesitisha kuajiri. Kumegeuka kuzuka kwa lawama kuhusiana na serikali ya awamu tano. Hakuna tatizo hapo. Tatizo ni mazoea ambayo watanzania tumekuwa nayo. Watanzania tulio wengi tunaamini sana katika kuajiriwa lakini si  
kujiajiri. Mfano Mtanzania yuko tayari kufanya kazi ambayo atalipwa mshahara wa laki moja na nusu kwa mwezi, kuliko  kuwekeza kwenye sekta nyingine ambapo angepata fedha nyingi zaidi ya hiyo. Maisha yetu watanzania yametaliwa na hofu. Mara nyingi huwa tuna hali ya kutojiamini, hali ambayo imepelekea kuishi kwa mazoea zoea. Timu zetu pia zina mazoea zoea tu. Usitegemee kupata miujiza kutoka kwenye timu zetu kwa sababu zinaendeshwa na watanzania ambao wanaishi kwa mazoea. Simba kwa sasa ipo Uturuki. Hakuna jambo la ajabu hapo. Simba kwa sasa iko katika chini ya mikono ya Mo'. Suala la uendeshwaji wa klabu 
Simba linaongozwa na Mo' na si wanachama. Simba ya sasa inaonekana ina kikosi imara. Simba imetwaa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita. Simba haijawahi kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa kwa siku za hivi karibuni. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003. Kuanzia hapo timu za Simba, Yanga, pamoja na Azam zimekuwa zikishiriki michuano hii ya kimataifa kwa mazoea zoea tu. Michuano hii mikubwa ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu sidhani kama timu zetu huwa wanaiheshimu na kuipa kipaumbele. Mechi nyingi za nyumbani huwa zinachezwa kwa masihara sihara sana. Timu zetu maranyingi huwa zinaambulia ushindi mwembamb 
a wa 1-0, 2-1, au sare ya 0-0, 1-1. Ushindi mabao 3-0 au 4-0 huwa unapatikana endapo kama Simba Yanga au Azam zinapocheza na timu za Djibout, Burundi, au Visiwa vya Sheli Sheli. Baada ya hapo timu zetu hupangwa na timu za Kasikazini au Magharibi mwa bara la Afrika. Na hapo ndipo utakapoanza kugundua masihara pamoja na mazoea ambayo watanzania wanayo. Timu zetu huwa zinatengeneza nafasi nyingi wakati zinacheza katika mechi za nyumbani. Kutokana na masihara pamoja na mazoea ambayo wachezaji wetu wanayo,  timu zetu huambulia kupata ushindi mwembamba. Timu zetu hazijawahi kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya
timu za kiarabu au Afrika magharibi. Badala yake timu zetu ndizo huenda kufungwa idadi kubwa ya magoli pale zinapoenda kucheza ugenini. Kuna sehemu hizi timu zinakosea. Mwakani Simba na Mtibwa Sugar watatuwakilisha katika michuano ya kimataifa. Kufika mbali kwa timu hizi katika michuano hii itategemea na wachezaji wazoefu walio nao ambao michuano hii wao si michuano migeni. Simba huenda ikafika hatua ya makundi hapo mwakani endapo kama watachanga karata zao vizuri. Mtibwa Sugar siwaoni wakifika mbali. Hakuna maandalizi yeyote makubwa ambayo yanafanywa kwa ajili ya mechi za mwakani. Historia itaongea.
LihatTutupKomentar