POGBA NA LACAZETTE WANA REKODI TAMU NDANI YA EPL

Na MOSES FRANCIS
+255715878724
Kiungo wa Manchester United Paulo Pogba na mshambuliaji wa Arsenal Alexander Lacazette wana zali la mentali. Ni zali la mentali ambalo ni zaidi ya lile alilowahi kulipata mbunge wa Mikumi mheshimiwa Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay. Sasa inshu iko hivi Paulo Pogba amejiandikia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa ligi kuu Uingereza kufunga goli la kwanza katika msimu mpya wa 2018/2019. Pogba amefanya hivyo katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Leicester City ambapo aliipatia timu yake ya Manchester United bao la kuongoza ndani ya dakika ya 3 tu ya mchezo. Kwa upande wa Lacazette naye inshu iko vile tu.Unaikumbuka mechi ya ufunguzi wa ligi kuu Uingereza msimu uliopita?. Kama hukumbuki basi nakukumbusha ilikuwa ni mechi kati ya Arsenal dhidi ya Leicester City. Ni mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa Emirates na tulishuhudia jumla ya mabao 7 katika mechi hiyo  ya ufunguziGoli la kwanza katika mechi hiyo lilifungwa na Alexander Lacazette dakika ya 2 tu ya mchezo  kwa kichwa akipokea pasi safi kutoka kwa kiungo Mohamed Elnemy. Kwahiyo Pogba na mwenzake Lacazette wanakuwa wachezaji raia wa ufaransa kufunga magoli katika mechi za ufunguzi za ligi kuu England. Rekodi hiyo haiishii hapo tu pia Pogba na mwenzake Lacazette wamefunga magoli yao ya ufunguzi wakitumia mchache zaid. Pogba yeye katumia dakika 3 tu kucheka na nyavu wakati mwenzake Lacazette yeye katumia dakika 2 tu za mchezo kufunga goli. Rekodi hii haiishii hapo hapo tu pia Pogba na mwenzake Lacazette wamefunga magoli yao katika mechi ya ufunguzi dhidi ya timu moja ambayo ni Leicester City. Patamu hapo.

LihatTutupKomentar