MBADALA WA RONALDO MADRID ATACHELEWA LAKINI YUPO.

Kwa sasa wako kimya. Wameamua kuiacha kwanza dunia ihangaike. Wako kimya. Vikao vyao vya bodi vinafanyika kimya kimya tu. Maskauti wao pia wanafanya kazi yao kimya kimya tu. Wamewaacha wadau wa soka pamoja na wachambuzi wa soka kama sisi tusijue walifanyalo. Ndio si kila ulifanyalo lazima utoe taarifa kwa umma, mambo mengine hufanyika kimya kimya tu. Ni kama utafiti wa kipelelezi ufanywao na maaskari wa FBI pale Marekani au CID hapa Tanzania. Mambo hufanyika kimya kimya tena hutawaliwa na usiri mkubwa. Katika jiji la Madrid kuna watu wanafanya mambo yao kimya kimya tu kwa sasa. Hawataki kuitaarifu duniakinachoendelea kwa sasa. Dunia itafahamishwa hapo baadae muda utakapofika lakini si sasa. Watu hawa ni rais wa Real Madrid Florentino Perez pamoja na mkurugenzi mtendaji Jose Angels Sanchez. Wanaume hawa wanajua fika wanaenda kuanza msimu mpya wakiwa hawana Ronaldo. Ndio jina la Ronaldo kwa sasa linapatikana katika kikosi cha Juventus pale Italia. Hali hii ndio inawafanya wakae kimya kwanza wavute nguvu ndipo baadae waje waishangaze dunia hapo baadae. Ronaldo kaondoka na mabao yake pale Madrid. Msimu uliopita Ronaldo na miaka yake 33 alifanikiwa kushika nafasi ya 2 nyuma ya Lione Messi akiwa amefungamagoli 26. Gareth Bale yeye na miaka yake 29  alishika nafasi ya 7 katika orodha ya wafungaji bora msimu uliopita akifunga magoli 16 tu. Karim Benzema yeye na miaka yake 30 alimaliza msimu akiwa hajafikisha hata goli 10. Hali hii ndio inaifanya bodi ya Real Madrid ikiongozwa na Florentino Perez iamue kumtafuta mbadala wa Ronaldo kimya kimya kwanza. Dunia itafahamishwa pale itakapofika tarehe 27 au 30 mwezi August mwaka huu. Ni kipindi ambacho usajili utakuwa umefungwa kwa ligi mbali mbali barani Ulaya. Kwa sasa ni suala la kukaa na kusubiri na kuona ni jina la mshambuliaji gani ambalo limependekezwana akina Jose Angels Sanchez. Tayari wameanza na golikipa Thibar Courtious kutoka katika klabu ya Chelsea. Kuna jina kubwa la mshambuliaji ambalo pia litafuatia baadae pale Real Madrid. Sitaki kuamini sana kuwa Real Madrid msimu ujao itaanza na Benzema na Bale pekee. Washambuliaji ambao hawawezi kufikisha magoli 30 ndani ya msimu mmoja. Kwa sasa tuendeleeni tu kubashiri kuwa huenda akawa ni Eden Hazard, Neymar, Antonio Griezman, Klian Mbappe, Edson Cavan au Harry kane. Mmoja Wapo kati ya hawa huenda akaenda kuvaa viatu vya Ronaldo ifikapo mwisho wa mwezi August mwaka huu. Tukaeni kimya na sisi tusubiri.

LihatTutupKomentar