LIGI YETU IMEANZA, LAKINI MABADILIKO BADO HAYAJAANZA.

Na
MOSES FRANCIS+255715878724

Simba dhidi ya Tanzania Prisons ni pambano la mechi ya ufunguzi ya ligi kuu Tanzania bara. Ni pambano ambalo litachezwa masaa machache katika uwanja wa taifa. Ni msimu mpya wa ligi kuu wa mwaka 2018/2019. Ni msimu ambao bingwa mpya wa msimu ujao anaanza kutafutwa kuanzia siku ya leo. Ni msimu mpya wa ligi ambao utachekesha na kubakisha  timu 16 tu mpaka ifikapo mwezi May mwakani. Timu nne zitashuka daraja na kurudi katika ligi daraja la kwanza. Bingwa wa ligi yetu amekuwa akipatikana kiunja ujanja tu. Ndio ni ujanja ujanja tu. Ligi yetu haiendeshwi kwa kufuata misingi ya weledi. Timu zetu haziendeshwi 

kwa kufuata misingi ya weledi. Mara nyingi uendeshaji wa timu zetu umekuwa ukifanywa kisela sela tu. TFF wamekuwa wakipangua ratiba ya ligi kuu pasipo kuwa na sababu za mashiko. Hili ni tatizo kubwa lakini limeonekana kama ni jambo la kawaida tu. Tuna safari ndefu sana. Mwezi ujao Taifa Stars itacheza pambano muhimu dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kuwania kombe la Afcon mwaka 2019. Huenda ni pambano ambalo litasimamisha ligi yetu kwa siku 10 hadi 13. Maandali ya timu ya taifa ambayo yangepaswa kutumia siku 5 yatachukua hadi siku 8. Kuna mahala ambapo tunazidi kukosea kila siku na tutaendelea kukosea tu.
Haya tuachane na hilo. Kuna hili jingine. Hili ndio kubwa na linaudhi na kukera. Azam ndio timu yenye kikosi bora cha vijana kwa sasa nchini. Shaban Idd Chilunda, Aboubakar Sure Boy Jr, Farid Musa, ni zao la Azam. Vilabu vyetu vya kariakoo nina mashaka kama vina timu nzuri za vijana kwa sasa. Hakuna. Ligi yetu inazidi kuwa na rundo kubwa ya wachezaji wengi wa kigeni kwasababu moja tu. Tumeshindwa kuwandaa wachezaji vijana katika misingi sahihi tangu wakiwa umri mdogo wa miaka 7, 11, 15, 17, na 20. Hawa vijana kila siku tunaishi nao majumbani kwetu tena kuna wengine tunawapita mitaani. Kinachotakiwa hapo  kinachotakiwa hapo ni kuwa na watu wenye jicho la uwezo wa ziada wa kuona na kubaini vipaji vya soka. Hebu jiulize kwa sasa katika klabu ya Simba kuna mshambuliaji kinda kutoka timu B ambaye anaandaliwa kuja kuwa Okwi wa baadae?. Hakuna. Kwa sasa katika klabu ya Yanga kuna mshambuliaji kinda kutoka timu B ambaye anaandaliwa kuwa Tambwe wa baadae? Hakuna. Tumekuwa tukiishi kwa mazoea sana hasa linapokuja suala la kuongoza mpira wetu hapa nchini. Nadhani kuna somo moja tunafeli na tutaendelea kufeli kama tusipofuata mifumo sahihi ya kuendeshaji wa soka. Somo hilo linaitwa weledi.

LihatTutupKomentar