KOCHA T-STARS AWAONDOA MASTAA WA SIMBA KIKOSINI

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania raia wa Nigeria Emmanuel Amunike leo kupitia kwa katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao ametangaza maamuzi mazito kuhusiana na wachezaji wa Simba SC waliokuwa wameitwa Taifa Stars.
Kocha Emmanuel Amunike kupita kwa katibu Kidao amewaondoa wachezaji wa Simba SC Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Shiza Kichuya, Hassan Dilunga na Jonas Mkude kwa kushindwa kufika katika kambi ya Taifa Stars kwa muda waliopangiwa bila sababu za msingi.
Baada ya kuondolewa kwa wachezaji hao na kubakia Aishi Manula pekee aliyekubali kuwasili kambini kwa wakati na hatimae wasiofika nafasi zao zimezibwa na Salum Kimenya, Salum Kihimbwa, Paul Ngalema, David Mwantika, Frank Domayo na Kelvin Sabato.

LihatTutupKomentar