ADAM SALAMBA AWA GUMZO KWA WAARABU

Baada ya kupiga tizi la nguvu kwa takribani wiki moja na nusu, kikosi cha Simba jana kimecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mouloudia ya Morocco na kwenda sare ya 1-1.

Katika mchezo huo uliovunjika mnamo dakika ya 65 ya kipindi cha pili kutokana na mvuak kali kuanza kunyesha, Mouludia walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 55.

Baada ya wapinzani kuapata bao la kuongoza, Simba walikuja juu wakionesha soka la kuelewana zaidi huku mbele wakianza Kagere na Okwi, walifanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Adam Salamba katika dakika ya 61.

Katika mchezo huo Simba walitumia mfumo wa kujilinda wa 4-4-2 ambao Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems, aliamua kuutumia kwa lengo mahususi la kukipima kikosi chake.

Kikosi cha Simba kilichoanza kiliwa na wachezaji, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, James Kotei, Sergi Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Clatous Chama, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na Hassan Dilunga.

LihatTutupKomentar