UBERIGIJI HAWAJA BAHATISHA KUMPIGA BRAZIL


Brazil imepoteza mchezo wa robo fainali dhidi ya Ubeligiji waliokuwa bora uwanjani. Licha ya umahiri wa Brazil katika kumiliki mpira lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya vijana wa Ubeligiji walionyesha kandanda safi na la kuvutia.

Pengo la Casemiro eneo la kiungo lilichangia kwa kiasi kikubwa kwa wateule ‘ Selecao ‘ kupoteza mchezo wa jana baada ya kumkosa mtu wa kutibua mipango ya Ubeligiji eneo la kiungo. Debryune alicheza huru na kuipanga Ubeligiji atakavyo.

Ni moja ya mechi bora tumepata kuitazama kabla ya fainali za michuano hiyo. Brazil walikuwa bora hususani dakika 20 za mwisho lakini Ubeligiji waliendelea kuwa bora na kuwazuia Brazil wasitibue ushindi wao wa 2-1.

“ walikuwa bora dhidi yetu. Tulijitahidi kupanga mipango mingi ya ushindi lakini ubora wao kwenye kiungo na safu ya ulinzi pia kukosa bahati ya ushindi vimetufanya kupoteza mchezo huo ‘ Miranda

BIG UP BELGIUM
Nawatizama kama mabingwa watarajiwa kombe la dunia 2018.

Unapopoteza mechi dhidi ya timu nzuri ama kwa hakika unajifunza mengi kimbinu na kiufundi pia kisaikolojia.


LihatTutupKomentar