SHABAN IDD CHILUNDA AANZA MAISHA YAKE MAPYA YA SOKA




Mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Idd Chilunda, amesajiliwa na CD Tenerife inayoshiriki Segunda Division (ligi daraja la kwanza).
Meneja wa Azam FC Philip Alando amethibitisha Chilunda amesaini mkataba wa miaka miwili na Tenerife.
“Ni kweli Chilunda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Tenerife. Amesaini mkataba huo siku mbili zikizopita”-Alando.
Chilunda ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Tenerife kutoka Azam baada ya klabu hiyo kumsajili Farid Musa.

LihatTutupKomentar