SAFARI YA SAMATTA ITAISHIA WEST HAM.

Na MOSES FRANCIS
+255715878724

Ukiwa katika jiji la New York nchini Marekani  hasa katika maeneo ya Forest Hills. Huwa kuna kaburi la mtu mashuhuri ambaye wamarekani pamoja na mimi tutaendelea kumkumbuka. Anaitwa DALE CARNEGIE huyu ni mwandishi wa vitabu mashuhuri ambaye alifariki miaka 63 iliyopita.  Wakati wa uhai wake aliwahi kusema kuwa "Kama Unataka Kuishinda Hofu Usikae Nyumbani  Na Kuiwaza Hofu Hiyo Bali Ni Kudiriki Kwa Kuanza Kuishinda Hofu Hiyo." Dale alikuwa yuko sahihi. Huwezi ukapata uzoefu wa kupambana na mnyama simba au chui kwa kukaa nyumbani tu. Ni kutoka na kuwafuata Simba au Chui huko waliko. Watanzania tulio wengi tuna hofu katika nafsi zetu. Akili zetu zimetawaliwa na hofu ya kushindwa, hofu ya kuchekwa, hofu ya kusemwa. Wachezaji wetu pamoja na mawakala wao pia wana hofu kubwa. Walio wengi huwa wanaanza harakati za kuishinda hofu tayari wakiwa wameshachelewa. Mfano Simon Happygod  Msuva kwa sasa ana miaka 25 kwa sasa. Ni umri ambao alipaswa umpate akiwa Ulaya. Wachezaji wetu huwa wana hofu sana na maisha yao. Mfano mchezaji wa Simba au Yanga hawezi akaacha mshahara wa milioni 2 kwa mwezi halafu akaenda kucheza soka ligi daraja la barani Ulaya kwa nchi kama Denmark, Scotland, au Sweden. Mawakala wao nao ni hivyo tu. Ni ngumu kwa wakala wa Mohamed Hussen kubeba CD zake na kuzipeleka katika klabu ya Kaizer Chiefs. Hiyo ni hofu. Mbwana Samatta kwa sasa ana miaka 26 ni umri ambao alipaswa awe  Ulaya timu kubwa lakini si Genk. Hebu jaribu kufikiria Mbwana Samatta amewazidi mwaka mmoja  Romelu Lukaku  Harry Kane ambao wao wanachezea timu kubwa Manchester United na Tottenharm. Kevin De Bruyne alipita Genk ambapo yupo Samatta kwa sasa akiwa na miaka 21 na sasa ana miaka 27 yupo zake Man City. Sitaki kuamini sana kuwa wachezaji wa Afrika huwa wanachelewa kuonwa vipaji vyao na mawakala wa Ulaya hapana. Bali Kuna  wakati mchezaji yeye kama yeye aanze safari ya kuanza kucheza barani Ulaya. Wachezaji wote wa Afrika Magharibi huwa wanaanza safari zao za soka kwa kuzamia tu. Huwa hawasubiri washikwe mkono au wapigiwe simu. Kuna ofa mbalimbali ambazo zinatolewa na timu mbalimbali za Ulaya zikimhitaji Mbwana Samatta. Lakini tusitarajie kumwona akivaa jezi ya Liverpool au Manchester United. Ili aweze kufika kwenye hizi timu itabidi imchukue miaka minne au mitano ambapo umri utakuwa umemtupa. Kuna uwezekano Samatta akapambana akafikia vilabu kama West Ham United. Ni ngumu kwa Samatta kuvuka hapo.

LihatTutupKomentar