PALE JUVENTUS INAPOTEMBELEA NYOTA YA RONALDO.


Na:MOSES FRANCIS
0743243120
Timu ya taifa ya Ufaransa imetinga hatua ya fainali katika michuano ya kombe la dunia pale Russia. Inshu ya Ufaransa si habari ya mjini katika vyombo vya habari hasa katika  mitandao ya kijamii. Inshu ambayo imeonekana kuteka hisia za wadau wengi wa soka ni uhamisho wa Cristian Ronaldo kwenda Juventus. Uhamisho huu mwanzoni ulionekana kama sinema, wengi walikuwa hawaamini kama Ronaldo ataondoka La Liga siku za hivi karibuni. Lakini badae Giusseppe Marotta, mkurugenzi wa klabu ya Juventus wamebadili kauli zetu na mitazamo yetu kama tulivyokuwa tunadhania kuhusu Cristian Ronaldo. Wamepeleka dau nono kwa Florentino Perez ambaye kakubali kuwauzia Ronaldo. Mpaka hapo kuna kitu lazima tujiulize. Juventus wanamsajili Ronaldo kwa lengo gani? Je ni kwa ajili ya kuwapa ubingwa wa Ulaya? au ni njia mojawapo ya kuitangaza klabu ya Juventus?. Lakini pamoja na yote haya nadhani swali la kwanza ndio ambalo litakuwa na mashiko zaidi. Mwaka 1985 ndio ulikuwa mwaka wa mwisho wa klabu ya Juventus kutwaa ubingwa wa Ulaya pale katika jiji la Brussels nchini Ubelgiji. Baada ya hapo Juventus hawajatwaa tena kombe la klabu bingwa barani Ulaya katika maisha yao yote. Hii ni historia mbaya inayouzi kunako katika klabu ya Juventus na hawataki tena kuiona ikiendelea katika vitabu vyao. Juventus wamecheza fainali 9 katika fainali za klabu bingwa barani Ulaya, wameshinda fainali moja tu ya mwaka 1985 zilizobaki zote 8 wamepigwa. Wamiliki wa Juventus familia ya Agnelli ilijitutumua kununua wachezaji nyota kutoka nje na Italia ili kuja kufuta aibu hii ya kutokutwaa ubingwa wa Ulaya kwa takribani muda wa miaka 33, umri wa Cristian Ronaldo. Carlos Tevez, Paulo Pogba, Gonzalo Higuain, Paulo Dyabala, ni baadhi ya wachezaji ambao wameonekana kushindwa kuipa Juventus ubingwa wa Ulaya. Wamiliki wa klabu ya Juventus wanatambua kuhusu kasi ya Ronaldo ambayo imepungua. Ronaldo wa sasa hawezi akakimbia na mpira kutoka katikati ya uwanja hadi golini na akafunga goli. Ronaldo huyu kwa sasa hawezi, ni mshambuliaji ambaye amekuwa akitumia akili nyingi na si nguvu kama ilivyokuwa hapo awali. Ronaldo huyu huyu kaipa ubingwa wa Euro timu yake ya taifa ya Ureno akiwa na miaka 31 na makombe matatu ya klabu bingwa akiwa na klabu yake ya Real Madrid. Hapa ndipo wamiliki wa Juventus wanapoanza kujiaminisha huenda wakatwaa ubingwa wa Ulaya kupitia mgongo wa Cristian Ronaldo, mshambuliaji ambaye ameonekana kuwa na bahati na michuano ya Ulaya.
LihatTutupKomentar