MZIMU WA VIONGOZI WA YANGA KUACHIA UONGOZI WAENDELEA CHARLES B MKWASA NAE AMEJIUZULU

KATIBU Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, amejiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na kilichodaiwa sababu za kiafya na wakati wowote kuanzia sasa atakabidhi barua ya uamuzi wake huo.
Mkwasa alianza kuitumikia Yanga SC kama mchezaji miaka ya 1980 na baadaye kuwa kocha kabla ya kuingia kwenye uongozi miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na MKOMESPORTNEWS Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Mustaph Ulungo, alisema Mkwasa ameshauriwa kupumzika na daktari wake na tayari amemtaarifu Kaimu Mwenyekiti wa klabu yao, Clement Sanga, juu ya uamuzi wake huo.
“Hospitali ameshauriwa kupumzika hivyo ametoa taarifa kwa uongozi, tumepokea barua yake iliyotumwa kwa Sanga,” alisema Ulungo.
Kuondoka kwa Mkwasa kumeacha maswali yaliyokosa majibu kwani pamoja na sababu alizozitoa, kulikuwa na habari za nyota huyo wa zamani Jangwani kutoelewana na baadhi ya wajumbe wa kamati za klabu hiyo, ikiwamo ya utendaji, usajili na mashindano.
Mkomesportnews  lilipomtafuta Mkwasa kuzungumzia juu ya uamuzi wake huo, muda wote simu yake iliita bila kupokewa.
LihatTutupKomentar