MBWANA SAMATTA KAFANIKIWA DIAMOND PLATNUM BAD

Na MOSES FRANCIS
+255715878724
Mr Nice yuko hoi. Ni kweli yuko hoi hakuna anayemkumbuka tena. Hakuna cha maana ambacho amekipata kutokana na kazi yake ya mziki tofauti  na umaarufu. Huwa ninasikia sikia miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wanaoishi maisha duni kwa sasa Mr Nice ni mmoja wao. Maisha yanakwenda kasi sana. Mwaka 2003 klabu ya Simba ilifanikiwa kuitoa klabu ya National El Ahly pale Cairo. Miongoni mwa wachezaji walioenda kupiga penati na kuzamisha jahazi la waarabu wa Misri ni beki Alex Massawe. Mungu amrehemu. Ametangulia mbele ya haki. Massawe alipatwa na mauti akiwa hana kitu, alikuwa yuko hoi kama alivyo Mr Nice kwa sasa. Maisha huwa ni kama  mshale wa saa. Maranyingi huwa haurudi nyuma huwa unasonga mbele tu. Msanii wa kizazi kipya Diamond Platinum kaanza kuimba mimi nikiwa nasoma  sekondari pale Shinyanga. Kwa haraka haraka ni kama miaka 10  tu kurudi nyuma. Ukienda Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, Kenya, Kongo, na hata Marekani msanii Diamond anajulikana. Diamond Platinum kashajitengenezea jina kubwa kwasasa ndani na nje ya bara la Afrika. Sitaki kuizungumzia sana menejimenti inayomsimamia Diamond Platinum. Lakini kifupi tu ni kwamba Diamond kashatambua njia sahihi ya kupita. Anafanya mziki kazi kama zilivyo
kazi nyingine. Hafanyi mziki wa kuburudisha hadhira kwa walivyo kuwa wanafanya kina Mr Nice enzi zao. Diamond Platinum kwa sasa anafanya show Marekani, Uingereza, na analipwa dola nyingi tu. Huwa nasikia sikia Diamond hawezi kufanya show yenye chini ya dola 15000 ambayo ni sawa na milioni 37. Diamond anajua kuna leo na kesho. Lakini pamoja na mafanikio yote haya ya  huyu kijana  aliyekulia Tandale bado kuna wasanii wengine wa Bongo Fleva hawajawa tayari kufuata njia aliyoifuata Diamond Platinum. Msanii kujitangaza kimataifa huwa inategemea na juhudi zake tu binafsi pamoja na menejimenti inayomsimamia.    Huwa hakuna uchawi mwingine zaidi ya hapo. Tatizo la wasanii wetu wa kibongo kuna baadhi yao hawataki kuwa chini ya menejimenti. Walio wengi huwa wanaamini watatusua wao kama wao tu. Ni ngumu katika soko la mziki kwa sasa ambapo mziki umegeuka kuwa biashara kubwa. Wasanii wakubwa wa Marekani kama kina R Kelly, 50 Cent, Rick Ross, na wengineo wamedumu kwenye gemu ya mziki kwa sababu wamezungukwa na watu sahihi (menejimenti nzuri). Kwa maana hiyo Diamond Platinum wasanii wenzake wameshindwa kumwelewa anachokifanya, labda huenda wanaona ni jambo la kawaida tu. Katika soka mambo kidogo yanaonekana kuwa ni tofauti kidogo. Tangu mshambuliaji Mbwana Samatta alipoamua kufanya maamuzi ya kwenda kucheza soka barani Ulaya ameacha matamanio kwa wachezaji wa nyumbani ambao nao wanataka kufikia mafanikio kama yakeAbdi Banda, Simon Msuva, Shaban Idd Chilunda, ni miongoni mwa wachezaji huenda wameshawishika na mafanikio aliyoyapata Samatta ndio maana na wao wameamua kufuata nyayo zake. Haya ndiyo maisha wanayotakiwa kuyafuata wasanii wetu pamoja na wachezaji wetu. Samatta yeye kashaleta ushawishi kwa wachezaji wetu, lakini Diamond Platinum yeye sidhani.

LihatTutupKomentar