HAWA WATOTO WAWEKA MALENGO YA KUIPELEKA TAIFA STARS KOMBE LA DUNIA

Raia wa Tanzania Laigwanani Mollel na Ziporah Godfrey Mollel walioshirikimichuano ya soka kimataifa ya Football for Friendship (F4F) wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakiwa na ndoto ya kuiwakilisha Tanzania katika Kombe laDunia siku moja.
Michuano hiyo ya F4F ilishirikisha watoto wenye miaka 12 kutoka nchi 211 naimefanyika kwa mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake.
Laigwanani na Ziporah wakitokea akademi ya Lengo Football ya Arusha Tanzania wameondoka Urusi kurejea Tanzaniawakisema ndoto yao kubwa ni kuiwakilishaTanzania katika Kombe la Dunia siku zausoni.
“Niiwakilisha vizuri Tanzania kwakupeperusha bendera ya taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Duniamwaka huu, ilikuwa kabla ya mechi yaufunguzi ya Urusi na Saudi Arabia.
“Nilikuwa na uchovu sana baada ya kazi yasiku ile lakini naamini nimepata hamasa ya kuiwakilisha nchi yangu katika Kombe laDunia siku zijazo kwa mimi mwenyewekucheza uwanjani,” alisema Laigwanani.
Kwa upande wake, Ziporah alisema; “Nitakua na faraja sana kwa sababuTanzania haijawahi kufuzu katika fainali zaKombe la Dunia, hivyo nitakuwa ni mimininaye iwakilisha nchi yangu.
“Nitajisikia ujasiri na nitaiwakilisha nchiyangu vizuri na najua katika mawazoyangu kuwa siku moja Tanzania itakuwahapa katika fainali za Kombe la Dunia.”
Program hii ya Kijamii ya F4F ni programu ya kijamii inayojumuisha siku tatu za mafunzo ya soka na kila timu kati ya timu32 kutoka duniani kote zilizipewa majinaya wanyama walio hatarini kupotea.
Timu zilizoundwa zilijumuisha wachezajikutoka kila pembe ya dunia, kutokamataifa makubwa na wadogo bila kujali,dini, tamaduni na ushawishi wa kisiasa nawa kiitikadi
LihatTutupKomentar