UHISPANIA YAMFUTA KAZI KOCHA WAO IKIWA IMESALIA SIKU MOJA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KUANZA

Uhispania imelazimika kumfuta kocha wake
Rais wa Shirikisho la Soka la Uhispania Luis Rubiales amesema shirikisho hilo "lililazimika" kumfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kukubali kujiunga na Real Madrid bila kuwafahamisha.
"Hii ni timu ya Uhispania, hauwezi kufanya mambo hivi," amesema.

Shirikisho la Soka la Uhispania limethibitisha kwamba limemfuta kazi meneja Julen Lopetegui ikiwa imesalia chini ya siku moja kabla ya michuano kuanza.
WamesemaJulen Lopetegui amefutwa na kwamba walifahamu kuwa alikuwa anajiunga na Real Madrid kuwa mrithi wa Zinedine Zidane dakika tano pekee kabla ya taarifa kutangazwa kwamba angekuwa meneja mpya wa klabu hiyo ya Madrid baada ya michuano hiyo.
Amesema huwa kuna utaratibu unaofaa kufuatwa wakati wa kuchukua hatua ya kutoa tangazo kama hilo.
"Tumelazimika kumfuta kazi mkufunzi wa timu ya taifa. Tunamtakia kila la heri," amesema rais wa shirikisho hilo Luis Rubiales.
LihatTutupKomentar