TETESI ZA USAJIRI ULAYA

Manchester United wako tayari kupambana na Manchester City na Real Madrid kumsajili mshambualiaji wa Ufaransa Kylian Mbappe 19, ambaye alikuwa akiichezea Paris St-Germain kwa mkopo kutoka Monaco. (Sunday Mirror)
Manchester United wanamuwinda beki wa kushoto wa Valencia na Uhispania Jose Luis Gaya, 23 baada ya dau la mchezaji waliokuwa wakimuwania Alex Sandro wa Juventus kuwa kubwa . (Sunday Mirror)
Manchester City imekuwa na makubaliano ya mdomo kuhusu kumsajili kiungo wa Napoli na timu ya taifa ya Italia, Jorginho, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.(Manchester Evening News)
Newcastle United haina haraka ya kumwachia mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic kuondoka St James' Park, huku timu hiyo ikitarajia kupata kitita kikubwa iwapo meneja Rafael Benitez bado anataka kumuuza .(Newcastle Chronicle)
Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas hajaamua kuanza tena mazungumzo na Liverpool kuhusu mchezaji Nabil Fekir, 24, lakini amesema kuwa mazungumzo hayo yamekwisha kwa sasa.. (Liverpool Echo)
Everton wanataka kumsajili mchezaji wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek, 22, na Jack Wilshere kutoka Arsenal.(Sunday Mirror)
Juventus pia inamuwania Wilshere-ambaye ataondoka uwanja wa Emirates mkataba wake utakapokamilika-huku Crystal Palace, West Ham na Wolves pia wakiwa wanamtaka mchezaji huyo. (Sun on Sunday)
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea ,Gunners, Olivier Giroud amesema kuwa kuondoka kwa Wilshere ni ''pigo kubwa''kwa Arsenal, akaongeza kuwa uamuzi wa kumuacha aende ni ''jukumu '' la Meneja Unai Emery. (Metro)
Inter Milan inawania sahihi ya winga Malcom kwa mkopo kutoka Bordeaux . (Football Italia)
Kiungo wa Croatia Mateo Kovacic, 24, anataka kuondoka Real Madrid na huenda akavutia vilabu vya Uingereza. (Marca)
Liverpool wako tayari kuungana na Barcelona kumuwania winga wa PSV Eindhoven,Hirving Lozano ambaye mustakabali wake utaamuliwa baada ya Kombe la dunia. (Star on Sunday)
West Ham inaripotiwa kusubiri jibu kutoka Lazio ili kuthibitisha mpango wake wa kumsajili mchezaji wake Felipe Anderson. (Football London)
Nahodha wa Brazili, Thiago Silva, amemtetea mchezaji mwenzie Neymar kuhusu kitendo chake cha kulia uanjani baada ya kushinda mchezo dhidi ya Costa Rica kwenye michuno ya kombe la dunia. ''Nilimwambia atoe yote aliyonayo moyoni, amekuwa akibeba mzigo mkubwa'', alisema Silva.
LihatTutupKomentar