TETESI ZA USAJIRI ULAYA

Borussia Dortmund ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Uhispania na Chelsea Alvaro Morata, lakini klabu hiyo ya Bundesliga inaweza ikashindwa kumsajili kutokana na mahitaji ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anayetaka kitita cha £45m(Bild, via Talksport)
Beki wa Uhispania Jordi Alba, 29, anasema kuwa anataka kusalia Barcelona, licha ya hamu kutoka kwa Tottenham. (goal)
Spurs ina matumaini ya kumsajili winger wa Croatia Ante Rebic, 24, huku klabu ya Eintracht Frankfurt ikitaka kumuuza kwa dau la £26.3m. (Bild, via Express)

Unamfahamu vipi kocha wa Senegal Aliou Cisse
Juventus inaongoza katika harakati za kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Urusi na CSKA Moscow Aleksandr Golovin, 22, huku Arsenal, Chelsea na Barcelona wakimnyatia. (Tuttosport - in Italian)

Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri ameanza kupanga kikosi chake cha ukufunzi katika klabu ya Chelsea licha ya hatma ya mkufunzi Antonio Conte kutotatuliwa (mail)
Lucas Torreira anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Sampdoria kwa dau la £26m, huku Arsenal ikimnyatia kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 22-kutoka Uruguay. (Sportitalia, via Mail)
Aston Villa haijapokea maombi yoyote kutoka kwa kiungo wa kati Jack Grealish, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhusishwa na Tottenham na Liverpool. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, ameshauriwa kujiunga na klabu ya ligi ya Marekani DC United na aliyekuwa mchezaji mwenza Steven Gerrard. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Sevilla na Argentina Ever Banega, 29, anataka hakikisho kutoka kwa mkufunzi wa Arsenal Unai Emery kabla ya kukubali kujiunga na klabu hiyo. (La Colina de Nervion, via Mirror)

Beki wa Uturuki na Freiburg Caglar Soyuncu, 22, anataka kujiunga na Arsenal. (Gunes, via Goal)

Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 30, anasema kuwa anapenda kujifurahisha na tayari amezungumza na wachezaji wenzake katika kikosi cha Ubelgiji nchini China na ligi ya Marekani MLS. (goal)

Klabu ya Fenerbahce imeanzisha mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25 Marco van Ginkel. (talksport)

Pendekezo la kipa wa Newcastle Matz Sels' kuelekea klabu ya Anderlecht limefutiliwa mbali baada ya klabu hiyo kukataa kukubali dau la uhamisho wa mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26.
LihatTutupKomentar