SVEN-GORAN HIVI AFRICA NI LINI TUTACHUKUA WORLD CUP

Wakati nilianza kazi kama kocha wa kikosi cha Ivory Coast nilimuambia Didier Drogba: "Tuna wachezaji wazuri, tunaweza kwenda mbali katika Kombe la Dunia, alisema: 'hapana hatuwezi'."
Sven-Goran Eriksson anajaribu kueleza ni kwa nini bado Afrika inasubiri kushinda kombe lake la kwanza la Dunia zaidi ya miaka 20 tangu nyota wa Brazil Pele atabiri mshindi kutoka Afrika ifikapo mwaka 2000. Hadi mwaka 2010 raia huyo wa Sweden alifahamu kuwa Drogba alisema ukweli.

"Sababu ambayo imechangia wazishinde ni neno moja tu: maandalizi," Erikson aliiambia BBC Spoti.
Wakati fulani utabiri wa pele ulionekana kutimia. Nigeria ilifika kileleni ikicheza na Argentina nyakati za Diego Maradona makala ya 1994, wakati wachezaji kama George Weah na Jay-Jay Okocha walikuwa wanawika huko Ulaya miaka ya tisini.
Lakini Afrika bara la pili lenye watu wengi zaidi duniani, ambapo kandanda imeenziwa, bado halijafanikiwa kuvuka robo fainali ya Kombe la Dunia.
Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia zitashiriki nchini Urusi baadaye mwezi huu lakini ni wachache wanaamini kuwa watakaribia fainali akiwemo mlinzi wa zamani wa Cameroon Luaren.
Hakuna timu kati ya tano za Afrika zinazoelekea Urusi ziko katika kundi la timu 20 za kwanza kwenye orodha ya Fifa, na Peter Odemwingie mshambuliaji wa zamani wa Nigeria anadai kandanda ya Afrika imedorora.
Nigeria ilikuwa na kikosi bora zaidi kutoka Afrika wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 1994. "Tulikuwa tunapisha mlangoni. Tulishinda kombe la olimpiki mwaka 1996 kwa kuwashinda Brazil na Argentina wakiwa na nyota wao wote.

"Wakati huo ilkuwa ni kama, 'ndio, linakuja'."
Lakini Nigeria ambao wanashiriki kombe lao la sita nchini Urusi bado wanasubiri.
Nchi ambazo zilifika robo fainali - Cameroon (1990) , Senegal (2002) na Ghana (2010) - zimetoka kusini mwa jangwa la Sahara.
Lakini wakati wa mashindano ya mwaka huu kutakuwa na timu nyingi kutoka kaskazini mwa Afrika kuliko eneo lolote barani ikiwemo inayoshiri mara ya kwanza kwa miaka 28 Misri, na inayorejea baada ya miaka 20 Morocco.
Baadhi ya nchi za Kaskazini mwa Afrika zina wachezaji waliojifunza kwenye taasisi za Ulaya, lakini ni Morocco wanaofika katika kombe hilo wakiwa na wachezaji wengi zaidi waliozaliwa nje ya nchi, ambapo 17 kati ya kikosi cha wachezaji 23 walizaliwa nje ya nchi.
Matatizo ya malipo na kususia mechi
Wakati wa kombe la Dunia la mwaka 2014 Cameroon, Ghana and Nigeria wote waligonga vichwa vya habari kwa sababu ambazo hazikuwa za kupendeza.
Wachezaji wa Ghana walisusia mazoezi wakilalamikia kutolipwa marupurupu yao huko Brazil.
Ilitatuliwa tu wakati serikali ilituma zaidi ya dola milioni 3 pesa taslimu kwa njia ya ndege.
'
Nao wachezaji wa Cameroon wakawasili wakiwa wamechelewa kwenye Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini kutokana na mzozo kuhusu malipo yao.
Shirikisho la kandanda nchini Nigeria lilisaini makubaliano na wachezaji Novemba iliyopita kuhusu malipo yao wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2018 kuzuia matatizo nchini Urusi.
Mlinzi wa zamani wa Tunisia Radhi Jaidi anaamini mizozo ya kifedha hutokana na ahadi zisizotimizwa.
'Ni Afrika na iko hivyo'
Eriksson alikuwa akiongoza kikosi cha Ivory Coast kilichoshiriki Kombe la Dunia la mwaka 2010.
Alikuwa na wachezaji wazuri wakiwemo Drogba na Salomon Kalou, ambao wote walikuwa wameishindia Chelsea kombe la Ligi ya Primia akiwemo pia kiungo wa kati Yaya Toure.
Lakini kocha huyo wa zamani wa Uingereza alikuwa na changamoto si haba alipokuwa akiandaa kikosi chake kwa mechi za makundi nchini Afrika Kusini dhidi ya Ureno, Brazil na Korea Kaskazini.
"Tulicheza mechi ya kirafiki na Switzerland na tulipoenda chumba cha kubadilishia nguo, hakukuwa na shati na ilikuwa imesalia saa moja na dakika 15 kabla ya mechi kuanza," Eriksson alisema.
"Nikauliza yuko wapi mtu wa nguo, nikaambiwa atakuja.

"Saa moja kabla, mtu wa nguo hakuwa amefika. Dakika 45 kabla, mtu wa nguo akafika na mikoba miwili mikubwa na kuiweka kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
Wachezaji wote wakavamia mikoba wakitafuta shati za kuwatosha. Kile nilichokisikia ni, 'Hili sio langu, Hili ni lako'.
"Kabla ya kuingia uwanjani mmoja wa wachezaji akaniambia, siwezi kucheza, nikauliza: umeumia? Akasema: Hapana, mtu wa nguo alisahau viatu vyangu.' Hoteli ilikuwa mbali na hakucheza.
"Drogba akaniambia: Sven, hii ni Afrika, Huwa iko hivyo.
"Wakati timu za Afrika zinacheza Kombe la Dunia, kawaida kuna fikra kuwa hawana fursa za kushinda.
"Tunastahili kuweka msingi wa kuwasaidia vijana wa Afrika ambao kwa sasa wako kati ya miaka 10 au 15 kuwasaidia kufikia viwango vya juu," anasema Jaidi.
Mlinzi wa Brighton na Cameroon Gaetan Bong anasema hata miundo msingi midogo inastahili kuboreshwa Afrika.
"Wakati mwingine huwezi kucheza kwa sababu uwanja ni mbaya," alisema. Tunastahili kujiimarisha zaidi kwa sababu tuna wachezaji wengi wenye vipawa barani Afrika lakini hatuna ligi zenye nguvu.
LihatTutupKomentar