SIMBA YAENDELEA NA MOTO ULE ULE YATINGA NUSU FINALI

Kikosi cha Simba kimefanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa matuta 3-2 dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya.
Mchezo uliokuwa uanpigwa Uwanja wa Afraha, umeshuhudiwa ukimalizika ndani ya dakika 90 huku kila timu ikishindwa kuona lango la timu pinzani.
Baada ya dakika 90 kumalizika hatua ya upigaji wa matuta ulifuatia na Simba ikaweza kupata penati mbili zilizofungwa na Erasto Nyoni, Haruna Niyonzima na Jonas Mkude.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa timu ya kwanza YA TANZANIA  kuingia nusu fainali baada ya Yanga na JKU zote kutolewa jana.
Baada ya Simba kuvuka robo fainali leo, Tanzania itawakilishwa tena na Singida United kesho katika Uwanja huohuo wa Afraha.
LihatTutupKomentar