MKWASSA "YANGA MSIMAMO WETU UPO PALEPALE"

Wakati Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akiwapiga Mkwara wa kuwapa saa 48 watafakari kuhusiana na maamuzi yao ya kutuma barua wakitaka kujiondoa kwenye mashindano ya KAGAME, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, amesisitiza hawatoshiriki.
Juzi Karia alisikika akisema kuwa Yanga wanapaswa kukaa na kujitafakari upya kutokana na maamuzi yao akieleza kuwa hayana mashiko, na akiwapa saa 48 pekee kutengua maamuzi yao.
Kwa mujibu wa Mkwasa, amesema kuwa kikosi chao kina wachezaji 7 pekee walio na mikataba huku wengine wote akieleza kuwa hawasaini na hivyo itakuwa ngumu kwao kushiriki mashindano hayo yanayotaraji kuanza Juni 28.
Mbali na wachezaji kukosa mikataba, Mkwasa amesema pia wachezaji wao wa kikosi cha pili wanashiriki mashindano ya Uhai CUP ambapo hawatoweza kutumika mara mbili.
"Hatuwezi kushiriki KAGAME sababu wachezaji wetu wapo likizo, wachezaji 7 tu ndiyo wana mikataba na wengine wote hawana. Wale wa kikosi cha pili wanashiriki Uhai CUP" alisema.
LihatTutupKomentar